SANAA YA TUPO SAWA
SANAA YA TUPO SAWA ni mradi ulioanzishwa na Taasisi ya Tupo Sawa Organization kwa lengo la kuwawezesha watu wenye ulemavu kiuchumi kupitia utoaji wa mafunzo ya ujuzi na stadi mbalimbali zitakazowafungulia fursa za kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea.
Programu ya mafunzo ya mradi huu imegawanyika katika makundi makuu mawili:
MAFUNZO YA USHONAJI (TAILORING TRAINING) – Kuwapatia washiriki ujuzi wa kushona na ushonaji wa mavazi ambao utawasaidia kuanzisha biashara zao wenyewe na kujipatia kipato.
MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI ZA MAJI (LIQUID SOAP MAKING TRAINING) – Kuwajengea washiriki uwezo na ujuzi wa kutengeneza sabuni za maji kama njia ya kujipatia kipato na fursa ya kujiajiri.
Kupitia mradi huu, Taasisi ya Tupo Sawa Organization inalenga kukuza uwezeshaji wa watu wenye ulemavu kiuchumi, kujitegemea, usawa wa fursa na ushirikishwaji wao katika jamii.
